1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Wapalestina wawili wauliwa Ukingo wa Magharibi

Josephat Charo
20 Juni 2023

Mpalestina mmoja amekufa leo kutokana na majeraha ya risasi aliyoyapata katika uvamizi uliofanywa mapema leo na Israel.

https://p.dw.com/p/4SqUi
Westjordanland | Israelischer Militäreinsatz in Jenin
Picha: Nedal Eshtayah/AA/picture alliance

Mpalestina mmoja amekufa leo kutokana na majeraha ya risasi aliyoyapata katika uvamizi uliofanywa mapema leo na Israel katika mji wa Jenin kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.

Taarifa ya wizara ya afya ya Palestina imesema Amjad Aref Jaas amekufa kutokana na majeraha mabaya ya risasi kwenye tumbo.

Baada ya mapigano kusita leo Jumatatu, wizara ya afya ya Palestina ilitangaza kuwa vikosi vya Israel vilimuua kijana wa umri wa miaka 20 karibu na mji wa Bethlehem katika Ukingo wa Magharibi.

Kijana huyo aliyetambuliwa kama Zakaria Mohammed al-Zaoul alipigwa risasi ya kichwa katika mji wa Husan.

Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vilikuwa katika doria ya kawaida mjini humo wakati mshukiwa mmoja alipowashambulia kwa mabomu ya kutengeneza nyumbani na wanajeshi wakajibu kwa risasi na kumjeruhi.