1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wa mazingira kuandamana nchi zaidi ya 50

Sylvia Mwehozi
15 Septemba 2023

Wanaharakati wa mazingira katika nchi zaidi ya 50 duniani kote wanatarajia kuanza maandamano leo yatakayodumu hadi Jumapili kuzishinikiza serikali kuachana na mafuta ya visukuku.

https://p.dw.com/p/4WMUR
Frankfurt | Fridays For Future Proteste
Picha: Michael Probst/AP/picture alliance

Wanaharakati wa mazingira katika nchi zaidi ya 50 duniani kote wanatarajia kuanza maandamano leo yatakayodumu hadi Jumapili. Maandamano hayo ya mwishoni mwa Juma yanalenga kuzishinikiza serikali za mataifa mbalimbali zisitishe uchomaji wa nishati ya visukuku inayochangia ongezeko la joto duniani.

Waratibu wake wanataka kuzieleza serikali kukomesha mara moja ruzuku za uchimbaji wa mafuta na gesi na kufuta mipango yoyote ya kupanua uzalishaji.Waandamana kushinikiza hatua za kunusuru dunia.

Maandamano hayo yanafanyika miezi miwili kabla ya mkutano wa kilele wa kimataifa wa mazingira COP28 huko Dubai, ambapo zaidi ya nchi 80 pia zitashinikiza makubaliano ya kuondoa hatua kwa hatua matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi. Mwaka huu kumeshuhudiwa ongezeko la vifo na athari za kiuchumi zinazotokana na majanga ya asili kama vile mafuriko, mioto ya nyika na ukame.