Wahamiaji 600 waingia kisiwa cha Italia cha Lampedusa
23 Machi 2024Matangazo
Mamlaka katika kisiwa hicho imesema kuwa jumla ya boti 13 zilisajiliwa ndani ya saa chache. Muda mfupi kabla ya kuwasili kisiwani humo boti moja iliyobeba wahamiaji 45, ilipata ajali ambapo watu wote walinusurika ispokuwa mtoto wa miezi 15 hajulikani alipo.
Maafa mabaya zaidi yamekuwa yajishuhudiwa mara kwa mara, wakati wahamiaji wakivuka bahari ya Mediterania wakijaribu kuingia Ulaya.
Kwa miaka kadhaa sasa kisiwa cha Lampedusa kilichopo kati ya kisiwa kingine cha Italia cha Sicily na taifa la Afrika Kaskazini la Tunisia kimekuwa ni kituo muhimu kwa wahamiaji wasio na vibali wanaofanya safari za kuifikia Ulaya.