Italia haijatimiza lengo la kudhibiti wahamiaji
1 Januari 2024Takwimu zilizotolewa na wizara yake zimeeleza kuwepo wahamiaji 155,750 walioingia nchini humo kwa mwaka 2023 pekee, ikiwa ni idadi tofauti na mwaka uliotangulia ambapo imetaja kulikua na wahamiaji 105, 000.Waziri huyo amesema idadi ya waliowasili kwa mwaka 2023, hailingani na mipango iliyowekwa kisiasa na kiserikali kama njia ya kupambana na wahamiaji haramu. Piantedosi amesifu ushirikiano uliofanywa na Tunisia na Libya wa kusaidia kukamatwa kwa maelfu ya wahamiaji.Kupunguza lindi la wahamiaji haramu wanaoingia nchini Italia ilikua ni mojawapo ya ajenda ya Waziri Mkuu Giorgia Meloni tangu aliposhika madaraka hayo mnamo Oktoba 2022.Wahamiaji husafiri kwa kutumia boti ambazo si salama kwa ushafirishaji abiria wa magendo wakitoka Tunisia na wengine Libya ambao hujaribu kuingia kisiwa cha Lampedusa, na Sicily.Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la wahamiaji IOM zaidi ya watu 2,750 waliotoweka kwenye makazi yao wanakadiriwa huenda wamefariki katika bahari ya Mediterania ndani ya mwaka mmoja, idadi inayotajwa kuwa ni kubwa zaidi ikilinganishwa na miaka mitano ilizopita.