1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa JKIA-Kenya wakubali kusitisha mgomo

11 Septemba 2024

Chama cha wafanyakazi wa mamlaka ya safari za ndege kimeridhia kuumaliza mgomo na kurudi kazini baada ya mgomo wa siku nzima uliosababisha kukwama kwa shughuli za safari za ndege.

https://p.dw.com/p/4kWEJ
Uwanja wa ndege wa JKIA Kenya
Uwanja wa ndege wa JKIA KenyaPicha: Billy Mutai/AA/picture alliance

Chama cha wafanyakazi wa mamlaka ya safari za ndege kimeridhia kuumaliza mgomo na kurudi kazini baada ya mgomo wa siku nzima uliosababisha kukwama kwa shughuli za safari za ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Nairobi wa JKIA. Hatua hiyo imetangazwa na katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini Kenya, COTU, Francis Atwoli ambaye amesema wafanyakazi wa mamlaka ya safari za ndege na serikali wamekubaliana juu ya kusitishwa kwa mgomo huo. Kuanzia usiku wa kuamkia leo shughuli zilikwama katika uwanja huo huku wasafiri wakibakia hawana la kufanya baada ya safari nyingi kufutwa na kucheleweshwa. Wafanyakazi wa JKIA walianzisha mgomo huo wakiishinikiza serikali iufute mpango wa kuipatia kampuni ya Adani kutoka India mamlaka ya kudhibiti uendeshaji wa uwanja huo kwa miaka 30.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW