EU yaridhia kuhusu sheria ya kurekebisha mazingira asilia
10 Novemba 2023Misitu zaidi inapaswa kuongezwa, viwanja kuruhusiwa kuota nyasi au miti asilia, na mito inapaswa kuruhusiwa kurudi kwenye mikondo yake ya awali.
Sheria hiyo ya Urejeshaji Uoto Asili ya Umoja wa Ulaya inaweka lengo kwa Umoja wa Ulaya kurejesha uoto uliokuwepo kwenye angalau asilimia 20 ya maeneo ya nchi kavu na bahari na mifumo yote ya ikolojia inayohitaji kushughulikiwa ifikapo mwaka 2050.
Wajumbe kutoka Bunge la Ulaya na kutoka nchi wanachama wa Umoja huo walikubaliana usiku wa Alhamisi juu ya mradi huo wa uhifadhi ulioshuhudia mjadala mkali.
Kulingana na takwimu za Umoja wa Ulaya, asilimia 80 ya makaazi asili ya viumbe hai katika umoja huo, yapo kwenye hali mbaya.
Aidha, asilimia 10 ya aina ya nyuki na vipepeo wapo katika hatari ya kutoweka huku asilimia 70 ya udongo umepoteza rutuba.