Viongozi wa kijeshi wa Niger kujibu uchokozi
4 Agosti 2023Hii ikiwa ni siku tatu kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho uliotolewa na jumuiya ya kikanda ya ECOWAS wa kurejesha utulivu.
ECOWAS ilikuwa imetishia uwezekano wa kutumia nguvu ikiwa viongozi wa kijeshi hawatomrejesha Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum ifikapo siku ya Jumapili. Jumuiya hiyo pia ilitangaza vikwazo vya kibiashara na kifedha baada ya mapinduzi.
Soma pia: Mtawala wa kijeshi Niger aonya dhidi ya uingiliaji wa kigeni na kuutaka umma kuilinda nchi
Viongozi wa mapinduzi pia wametangaza kuwasimamisha mabalozi katika nchi nne, pamoja na kufuta ushirikiano wa kijeshi baina ya nchi hiyo na Ufaransa. Mabalozi wa waliovuliwa majukumu ni katika nchi za Ufaransa, Nigeria, Togo na Marekani.
Uamuzi huo umetolewa wakati uongozi wa kijeshi ukizidi kukabiliwa na shinikizo la kumrejesha madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum.