1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege za uokozi kutoka Niger zatua Ufaransa

2 Agosti 2023

Ndege za kwanza zilizowabeba raia wa Ufaransa na raia wengine wa mataifa ya Ulaya waliohamishwa kutoka Niger, zimetua mjini Paris leo Jumatano, wiki moja baada ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4Ugah
Niger Evakuierung der ausländischen Staatsbürger/Niamey Flughafen
Picha: Stanislas Poyet/AFP

Kufikia mapema leo, karibu watu 500 walikuwa wamewasili mjini Paris, wakiwemo raia wengi wa Ufaransa, lakini pia Wareno, Wabelgiji, Wanaigeria, Waethiopia na raia kadhaa kutoka Lebanon. Wakati huo huo, ndege ya kijeshi iliyokuwa imewabeba raia wa Italia kutoka Niger imewasili leo alfajiri katika uwanja wa ndege wa Ciampino karibu na mji mkuu Rome. Antonio Tajani, Waziri wa mambo ya nje wa Italia amesema, "Lazima niseme hata ubalozi wa Marekani umeishukuru Italia kwa ufanisi wake katika zoezi hilo. Na natoa shukrani kwa kitengo kinachohusika na migogoro, ofisi ya ubalozi wetu nchini Niger, na pia jeshi letu kwa kuwarejesha nyumbani sio tu raia wa Italia bali wa nchi nyingine pia." Rais Mohamed Bazoum alizuiliwa na walinzi wake katika mapinduzi ya tatu ya kijeshi ndani ya miaka mitatu katika ukanda wa Sahel, kufuatia yale yaliyotokea kwenye nchi jirani za Mali na Burkina Faso.