1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Chadema waachiwa kwa dhamana

13 Agosti 2024

Viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Chadema, wameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kuelekea maandamano ya vijana yaliyokuwa yamepangwa kufanyika nchini humo.

https://p.dw.com/p/4jPPK
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema Freeman MbowePicha: ERICKY BONIPHACE/AFP

Viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Chadema, wameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kuelekea maandamano ya vijana yaliyokuwa yamepangwa kufanyika nchini humo. Haya yamesemwa leo na msemaji wa chama hicho John Mrema.

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, Mrema amesema mwenyekiti Freeman Mbowe na makamu wake Tundu Lissu, wamerejeshwa Dar es Salaam na maafisa wa polisi na wametoa dhamana. Msemaji huyo wa Chadema lakini amesema kuna ripoti kwamba baadhi ya viongozi wa tawi la vijana la Chadema, Bavicha, waliokuwa wamekamatwa, bado wanaendelea kushikiliwa na maafisa wa polisi mjini Mbeya.Wapinzani Tanzania walaani kukamatwa viongozi wao

Taarifa ya polisi ilisema watu 520 walio na mafungamano na chama hicho, wakiwemo viongozi na wanachama vijana, walikamatwa kuelekea mkutano huo wa siku ya vijana uliokuwa umepigwa marufuku.