1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Polisi nchini Uturuki wawazuia watu 33 wanaofungamana na IS

10 Machi 2024

Polisi nchini Uturuki wanawazuilia washukiwa 33 walio na mafungamano na kundi la Dola la Kiislamu waliokuwa wakipanga mashambulizi kabla ya uchaguzi wa serikali ya mitaa.

https://p.dw.com/p/4dMAB
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Ali Yerlikaya
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya akizungumza na waandishi wa habari mbele ya jengo la wizara hiyo baada ya shambulizi la bomu mjini Ankara, Oktoba 1, 2023.Picha: Cagla Gurdogan/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya amesema hayo wakati taifa hilo likijiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwezi huu.

Polisi ya kupambana na ugaidi katika mji wa Sakarya ulioko kaskazini magharibi mwa Uturuki walikamata silaha, fedha taslimu na kile walichokiita nyaraka za kundi hilo wakati wa msako.

Waziri huyo amesema mtandao huo ulikuwa ukiwapeleka wapiganaji katika maeneo ya kivita na msaada wa kifedha kwa IS wakati wakiendesha harakati zao katika misikiti na shule za kidini zisizotambulika.

Uturuki imekumbwa na mashambulizi mengi yanayohusishwa na IS katika kipindi cha miaka 10, likiwemo shambulizi la ufyatuaji risasi katika kanisa moja mjini Istanbul Januari 10 lililosababisha kifo cha mtu mmoja.