Taliban kutuma wajumbe wake kwenye mazungumzo ya Doha
17 Juni 2024Msemaji mkuu wa Taliban Zabihullah Mujahid anaamini kuwa, ushiriki wao katika kongamano hilo la siku mbili nchini Qatar kutaisaidia Afghanistan linapokuja suala la misaada ya kibinadamu na uwekezaji.
Kwa upande wake, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Taliban Abdul Qahar Balkhi amesema kuwa utawala huo umekubali kushiriki kongamano hilo baada ya kuitazama ajenda na orodha ya watu watakaoshiriki mkutano huo.
Soma pia: UN yalaani adhabu ya vibiko Afghanistan
Balkhi hata hivyo ameweka wazi kuwa kushiriki kwao ni kwa masharti. Iwapo kuna mabadiliko yoyote kwenye ajenda, basi Taliban huenda ikabadili uamuzi wao.
Kongamano hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu Afghanistan linafanyika mnamo Juni 30 na Julai mosi, kwa lengo la kuongezea ushirikiano wa kimataifa na nchi hiyo ambayo inakabiliwa na migogoro chungunzima.