1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfghanistan

UN yalaani adhabu ya vibiko Afghanistan

6 Juni 2024

Umoja wa Mataifa umelaani matukio ya kutoa adhabu ya uchapaji viboko nchini Afghanistan, na kutoa wito kwa mamlaka za Taliban kukomesha tabia hiyo.

https://p.dw.com/p/4gjCx
Adhabu ya uchapaji viboko Afghanistan
Taliban imeanza kutekeleza tena adhabu kali inazodai zinatokana na sheria za KiislamuPicha: AFP

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA, umesema takribani watu 63 walichapwa hadharani katika jimbo la kaskazini la Saripul siku ya Jumanne.

Kwenye ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X, ujumbe wa UNAMA ulilaani adhabu ya viboko na kuitaka Afghanistan kuheshimu majukumu yake ya kimataifa ya haki za binadamu.

Soma pia: Taliban yakaribisha uamuzi wa kuongezwa muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Afghanistan UNAMA

Tangu kurejea kwao madarakani mnamo takribani miaka mitatu iliyopita, serikali ya Taliban imeanza kutekeleza tena adhabu kali inazodai zinatokana na sheria za Kiislamu.

Miongoni mwa matukio hayo ni kualika umati wa watu kutazama visa vya kunyongwa hadharani na mateso ya kimwili, hawa kwa watu kupigwa mijeledi.

Hukumu hizo zimetekelezwa kwa washukiwa wa uhalifu ikiwa ni pamoja na wizi, uzinzi na unywaji wa pombe.