UN:Korea Kaskazini imehusika kupotea kwa watu
28 Machi 2023Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Korea Kaskazini ilichunguza kuongezeka kwa visa vya upoteaji wa watu,kutekwa nyara na kusema taifa hilo linapaswa kukiri limejihusisha na sera ya serikali ya kutekelezwa kwa vitendo hivyo tangu 1950.
Ofisi hiyo imeitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia visa hivyo, ilivyoyitaja ni uvunjifu wa haki za binadamu..
Ripoti hiyo iliotokana na mahojiano ya watu kadhaa wakiwemo waliotekeleza vitendo hivyo zamani wakiwa kama watekaji nyara.
Ndugu na jamaa wa wahanga wa matukio hayo ni sehemu ya waliohojiwa pia,wakielezea kwa kina namna watu walivyotoweka ikiwa ni pamoja na kuwekwa kizuizini kiholela nchini Korea Kaskazini.
Si tu raia wa Korea Kaskazini waliokutana na mikasa hiyo bali raia wa mataifa kama vile,Korea Kusini,Japan na kwingineko walitekwa nyara.
Soma pia:Umoja wa Mataifa yaitisha uchunguzi kufuatia mauaji ya Eswatini
Mkuu wa shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema kuongezeka kwa visa vya kutoweka kwa watu ni ukiukwaji mkubwa wa haki nyingi kwa wakati mmoja na jukumu hilo linasalia chini ya viombo vya dola vya taifa hilo.
"Natowa wito kwa Jamhuri ya watu wa Korea kutambua ukiukwaji huu na kuchukua hatua"
Alisema Turk na kutoa mwito kwa mataifa yote ulimwenguni kusaidia waathiriwa katika harakati zao za kusaka haki
Pyongyang yakanusha matokeo ya uchunguzi
Pyongyang imekanusha mara kwa mara tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu na kukosoa uchunguzi huo wa Umoja wa Mataifa.
Matokeo ya uchunguzi huo imeichukulia kama mpango unaoungwa mkono na Marekani kuingilia masuala yake ya ndani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo waathirika wengi wa visa vya kutoweka ndani ya Korea Kaskazini mara nyingi walipelekwa kwenye magereza maalum ya wafungwa wa kisiasa au sehemu zingine na kuwekwa kizuizini.
Ndugu:Tunahitaji kujua hatma ya jamaa zetu
Baadhi ya ndugu na jamaa wa waathiwa wanasema bado wanahitaji kujua hatma za wapendwa wao.Kim Jae Jo amewaambia wachunguzi wa ripoti hiyo.
"Uthibitisho wa hatma yake ni muhimu sana,sijui unanielewa?" KIm alimuuliza mmoja wa wachunguzi wa ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa.
Soma pia:Korea Kusini yaaita Korea Kaskazini "adui" baada ya miaka sita
Aliendelea kusema "nataka hatma yake ijulikane.Ikiwa amefariki dunia,ningependa mabaki yake yarudishwe."
Sehemu ya ripoti hiyo imeonesha udharura wa jumuiya ya kimataifa kuunganisha juhudi za pamoja,kuchunguza uhalifu dhidi ya binadamu uliotendeka kwenye taifa hilo lililojitenga.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol leo Jumanne amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuelewa linapokuja suala la ukiukwaji haki za binadamu huko Korea Kaskazini.
Ripori hiyo ya Umoja wa Mataifa inatolewa huku kukiwa na hali ya wasiwasi katika eneo hilo, baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiamuru kuongezwa kwa uzalishaji wa silaha za nyuklia na kusema nchi inapaswa kuwa tayari kutumia silaha hizo wakati wowote.