Tutaijibu Marekani kwa nyuklia - Pyongyang
4 Machi 2023Korea Kaskazini imeilaumu Marekani kwa kile ilichosema ni "kusambaratika kwa mifumo ya kimataifa ya udhibiti wa silaha" na kusisitiza kuwa silaha za nyuklia za Pyongyang ni jibu stahiki ili kuhakikisha amani na utulivu katika rasi ya Korea.
Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imesema kupitia shirika la habari la serikali, KCNA, kwamba Marekani, Korea Kusini na Japan wamekuwa wakivuka mstari mwekundu na kwamba hali hii kamwe haiwezi kuvumiliwa.
Soma zaidi: Marekani na Korea Kusini zatafakari kutanua Luteka za Kijeshi
Kim Jong Un aombwa kuzungumza na mrithi wake Suk Yeol
Hayo ni baada ya Marekani na Korea Kusini kutangaza hapo jana kuwa zitafanya luteka ya pamoja ya kijeshi ya siku 10, kuanzia Machi 13.
Mazoezi hayo ya kijeshi yamekuwa yakiibua hisia kali kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imekua ikitoa vitisho vya kutumia silaha za nyuklia.