1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kusini yaaita Korea Kaskazini "adui" baada ya miaka 6

16 Februari 2023

Korea Kusini imeitaja Korea Kaskazini kama adui yake katika waraka wa ulinzi iliouchapisha hii leo, ikiwa ni miaka sita tangu ilipolitumia neno "adui"

https://p.dw.com/p/4NZmo
Nordkorea Militärparade
Picha: KCNA/REUTERS

Hatua inayoashiria kuimarika kwa msimamo wa Korea Kusini kuelekea Pyongyang.

Sehemu ya waraka huo imesema kwa kuwa mwezi Disemba, Korea Kaskazini iliitaja Korea Kusini kama "adui wa kweli", na kwa hiyo Korea Kusini nayo inaiainisha serikali ya Korea Kaskazini na jeshi lake ambalo ndilo mtendaji mkuu wa shughuli zake kuwa ni adui wao.

Soma pia:Korea Kaskazini yaonyesha silaha zake katika gwaride

Wachambuzi wanasema, matamshi haya yanaashiria hali ya kimahusiano baina ya majirani hao na yanayorejesha hisia za enzi ya Vita Baridi.

Mataifa hayo mawili, kimsingi bado yako katikavita tangu vita vya Koreavya kati ya mwaka 1950 hadi 1953, vilivyomalizwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano badala ya makubaliano ya amani.