UNEA yakutana Nairobi kujadili ushirikiano dhidi ya migogoro
26 Februari 2024Matangazo
Kabla ya mkutano huo, Mkuu wa Mpango wa Kimataifa wa Mazingira (UNEP), Inger Andersen, ameliambia shirika la habari la AP kwamba hakuna binaadamu yeyote anayeishi peke yake na kwamba kila mtu anaishi katika sayari ya dunia.
"Kila mmoja lazima ashirikishweo kwa kuwa njia ya pekee ya kutatua baadhi ya matatizo hayo ni kwa mazungumzo ya pamoja." Alisema.
Mkutano huo katika mji mkuu wa Kenya ni kikao cha sita cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kinachohudhuriwa na nchi wanachama, mashirika ya kiraia, wanasayansi na sekta binafsi.
Katika mkutano huo, nchi wanachama hujadili rasimu za maazimio kuhusu masuala mbalimbali ambayo baraza hilo hupitisha baada ya makubaliano.