UN yasema msaada usio na kikomo unahitajika Gaza
27 Oktoba 2023Matangazo
Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa msaada usio na kikomo unahitajika Gaza ikiwa ni baada ya wiki tatu za mashambulizi ya Israel ya kulipiza mashambulizi ya Hamas mwezi huu ambayo yamechochea mgogoro wa kiutu katika ukanda huo unaozingirwa wa Kipalestina.
Kamishna mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA, Philippe Lazzarini, amesemamsaada wa kutosha unahitajika katika Ukanda wa Gaza, akisema msaada unaoingia kwa sasa ni kama makombo.
Soma pia:UN yasema msaada usio na kikomo wahitajika Gaza
Lazzarini pia amethibitisha kuwa wafanyakazi 57 wa shirika hilo wameuawa katika vita hivyo.