1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

UN Kupigia kura azimio la uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Hawa Bihoga
17 Februari 2023

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura juu azimio lililotolewa na Ukraine na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, ukiwa ni mwaka1 tangu Urusi ilipoanza mashambulizi yake.

https://p.dw.com/p/4NdyZ
USA UN-Sicherheitsrat
Picha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/IMAGO

Sehemu ya azimio la washirika hao ni pamoja na kutaka mipaka ya Ukraine iheshimiwe, kadhalika Urusi kuondoa vikosi vyake katika taifa hilo.

Azimio hilo la Kyiv na washirika wake wa Magharibihalioneshi mapendekezo maalum ya moja kwa mojakatika kuleta suluhu ya amani katika mgogoro huo uliogharimu maisha ya maelfu wa watu, huku mamilioni wakiyakimbia makaazi yao.

Badala yake, azimio hilo linasisitiza juu ya misimamo ambayo tayari imetolewa na nchi wananchama 193 wa Baraza Kuu, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono uhuru wa mipaka ya Ukraine na amri kwa Urusi kuondoa majeshi yake.

Baadhi ya wanadiplomasia wameliambia shirika la habari la dpa kwamba, azimio hilo ni mwangwi kwa baadhi ya maazimio yaliyopitishwa na Umoja wa Mataifa katika mkutano mkuu kuhusu mzozo huo.

Aidha wakisisitiza washirika wa Magharibihawapaswi kuweka mukhtasari tata katika mpango wa kumaliza mzozo kwa kupiga kura, lakini kwa kuhamasisha nchi nyingi iwezekanavyo kuunga mkono azimio hilo.

NATO yajadili jinsi ya kuipatia Ukraine silaha zaidi

Kikao cha Baraza hilo kinatarajiwa kuanza mapema juma lijalo na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wanatarajia kuhudhuria, huku Februari 24 ikiwa ni kumbukumbu ya uvamizi wa Urusi kwa Ukraine.

Soma pia:Ukraine yawaomba washirika wa NATO kuharakisha silaha

Viongozi mbalimbali wa dunia wanatarajiwa kuhutubia katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Rais wa China Xi Jinping ambaye hakuonesha kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine tangu mwanzo, nae atatoa hotuba yake kuhusu kusaka suluhu ya amani, amethibitisha  mwanadiplomasia mkuu wa China, Wang Yi.

Putin:watoto wameathirika wakati wa mzozo

Urusi ikiwa inadhibiti baadhi ya mikoa ya Ukraine na kuweka viongozi wake, Rais Vladimir Putin amemwambia Kamishna wake wa haki za watoto, Maria Lvova-Belova, kwamba kuna idadi kubwa ya maombi ya warusi wakitaka kuwaasili watoto kutoka mikoa ya Donetsk, Luhansk, Kherson na  Zaporizhzhia.

Wladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Pavel Bednyakov/Kremlin/REUTERS

Amemwambia taasisi ya Urusi kushughulikia masuala ya haki za watoto,imekuwa ikihusika na kufuatilia namna watoto wanavyoathirika kwa takriban miaka 9 wakati mzozo ulioanza kufukuta.

"Kinachotokea Donbas kwa bahati mbaya kinaathiri watoto wetu wadogo kwa miaka 8,bila shaka, watoto wameteseka."

Mikoa minne ya Ukraine ambayo ni pamoja na Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia  imedhibitiwa na Urusi mnamo Septemba, wakati ambapo mapambano kwenye uwanja wavita yakishamiri.

Soma pia:Urusi yashambulia maeneo ya jimbo la Donetsk

Putin alikaribisha maombi ya warusiambao wanataka kusaidia familia ambazo wapendwa wao walijiunga katika oparesheni maalum ya kijashi wakiwemo askari wa akiba, mpango uliokosolewa vikali na jumuia ya kimataifa na miongoni mwa warusi.