SiasaUrusi
Urusi kupunguza uzalishaji wa mafuta
10 Februari 2023Matangazo
Naibu Waziri Mkuu wa Urusi, Alexander Novak amesema Urusi itapunguza uzalishaji wa mafuta ghafi kwa kiwango cha asilimia tano kuanzia mwezi ujao ikiwa ni kukabliana na hatua ya mataifa ya magharibi ya kuweka ukomo wa bei.
Novak amesema kuanzia Machi, Urusi itapunguza uzalishaji wa mafuta mapipa 500,000 kwa siku. Hatua hiyo amaesema inakusudia kudumisha mahusiano ya soko.
Urusi ni sehemu ya muungano na matiafa yenye kuzalisha mafuta kwa wingi dubniani OPEC ambao hukutana mara kwa mara ili kuamua viwango vya pato la mafuta.
Kutokana na operesheni ya kijeshi ya serikali ya Moscow nchini Ukraine, nchi za Magharibi zimepunguza bei, hatua ambayo inailazimisha Urusi kuweza kuuza mafuta ghafi yake kwa kiwango cha chini.