1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Von der Leyen kuzuru Lampedusa

17 Septemba 2023

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen anatarajiwa kutembelea kisiwa cha Lampedusa nchini Italia hii leo baada ya kualikwa na waziri mkuu wa taifa hilo Georgia Meloni.

https://p.dw.com/p/4WRSz
Italien | Migranten auf Lampedusa
Boti iliyobeba wahamiaji ikiingia katika bandari ya Sicilian iliyopo kisiwa cha Lampedusa, Septemba 16,2023 ambako kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la wahamiaji hivi karibuni Picha: Cecilia Fabiano/AP Photo/picture alliance

Ursula von der Leyen anazuru eneo hilo wakati miito ya kushughulikia tatizo lililosababishwa na kuwasili kwa idadi kubwa ya wahamiaji katika mipaka ya Umoja wa Ulaya ikiongezeka.

Von der Leyen anakwenda Lampedusa baada ya kualikwa na waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni ambaye ataandamana naye kwenye ziara hiyo.

Kiongozi huyo wa mrengo mkali wa kulia Meloni ametoa wito wa kuanzishwa mara moja kwa operesheni za Umoja wa Ulaya za kuzizuia boti za wahamiaji na kuongeza kuwa kama kuna uwezekano lipelekwe jeshi la wanamaji.

Meloni na von der Leyen walizuru Tunisia kwa pamoja mwezi Juni, ambako ndiko kitovu cha wahamiaji kuanza safari kwenda Ulaya.