Ukraine yapuuzia kauli kuwa haijapata mafanikio vitani
29 Novemba 2023Matangazo
Akizungumza leo mjini Brussels ambako anahudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Jumuiya ya Kujihami - NATO, Kuleba amesema hakuna mkwamo wowote.
Kuleba amesema alitamani kuweka wazi kile ambacho mawaziri wenzake wamejadili katika mkutano, lakini amewahakikishia waandishi wa habari kwamba hakuna mkwamo wa kijeshi na njia iko wazi ya msaada zaidi kwa Ukraine.
Soma pia:Mawaziri wa NATO wakutana na kuahidi mshikamano na Ukraine
Kuleba anakutana na mawaziri wenzake wa NATO kujadili hali ilivyo katika uwanja wa vita na uungwaji mkono wa Kyiv kutoka nchi za Magharibi.
Kwa mara nyingine ametoa wito kwa wanachama wa NATO kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa silaha na vifaa vingine vya kijeshi ili kuiunga mkono Ukraine.