1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa NATO wajadili ushirikiano wa karibu na Ukraine

29 Novemba 2023

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanakutana leo na mwenzao wa Ukraine Dymitro Kuleba mjini Brussels kujadili hali katika uwanja wa vita mashariki na kusini mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4ZZR8
Ubelgiji | Mkutano wa NATO na Ukraine
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba akiwa na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg. Picha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanakutana leo na mwenzao wa Ukraine Dymitro Kuleba mjini Brussels kujadili hali ilivyo katika uwanja wa vita na uungwaji mkono wa Kyiv kutoka nchi za Magharibi.

Juhudi za Ukraine kuainisha vyombo vyake vya ulinzi na usalama na viwango vya NATO pia lipo kwenye mada kwa kuzingatia uwezekano wa Ukraine kujiunga na muungano huo wa kijeshi.

Soma pia: Wanachama wa NATO waahidi kuendelea kusimama na Ukraine

Akizungumza wakati akiwasili Brussels, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dymitro Kuleba aliondoa hofu kuwa jeshi la Ukraine halijapiga hatua katika vita vyake dhidi ya Urusi, akisema kuwa hakuna mwako wowote.

Amesema lengo la kimkakati la Ukraine la kuiokomboa ardhi yake, ikiwemo Rasi ya Crimea, halijabadilika na hakuna kitakachowazuia.