1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine na Urusi zabadilishana wafungwa wa kivita

14 Septemba 2024

Urusi imesema kuwa imebadilishana na Ukraine wanajeshi 103 wa Ukraine waliotekwa kwa idadi sawa ya askari wa Urusi chini ya usimamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

https://p.dw.com/p/4kd4d
Ukraine
Raia wa Ukraine ambao wameachiliwa na Urusi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mabadilishano baina ya nchi hizo mbiliPicha: Ukrainian Presidential Press Office/AP Photo/picture alliance

Urusi imesema leo kuwa imebadilishana na Ukraine wanajeshi 103 wa Ukraine waliotekwa kwa idadi sawa ya askari wa Urusi chini ya usimamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kulingana na wanajeshi wa Urusi walioachiliwa katika mabadilisho hayo walitekwa wakati wa uvamizi wa Ukraine katika eneo la Kursk, ambao ulianza Agosti 6 mwaka huu.

Soma zaidi. Stoltenberg asema NATO ingeweza kuisaidia zaidi Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy amethibitisha kuhusu mabadilishano hayo na kusema kwamba mabadilishano mengine yatafanyika ndani ya siku mbili zijazo.

Kwa upande wa wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wote wa Urusi waliorejeshwa na Ukraine wako kwenye eneo la Jamhuri ya Belarusi, ambapo huko wanapewa msaada muhimu wa kisaikolojia na matibabu.