1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yatoa tahadhari kwa raia wake Uganda

18 Oktoba 2023

Serikali ya Uingereza imetoa tahadhari kwa raia wake wajiepushe kuitembelea mbuga mashuhuri ya wanyama nchini Uganda ambako watalii wawili, akiwemo raia mmoja wa Uingereza, kuuawa.

https://p.dw.com/p/4XfwI
Uganda Kampala Bombenanschlag auf Kirche verhindert
Askari wa Uganda wakilinda eneo yalipofanyika mashambulizi kwenye jengo moja la kanisa.Picha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Maafisa wa polisi na wa mbuga ya wanyama wamesema watu hao watatu walishambuliwa siku ya Jumanne (Oktoba 17) na watu waliokuwa na bunduki wakati walipokuwa wakifanya safari katika mbuga ya kitaifa ya Malkia Elizabeth kusini magharibi mwa Uganda na gari yao kutiwa moto.

Shirika la Huduma za Wanyamapori la Uganda limewatambua wahanga wengine wawili kama mtalii wa Afrika Kusini na muongpzaji safari wa Uganda.

Soma zaidi: Polisi ya Uganda yatibua njama ya waasi kulipua makanisa

Polisi wamelinyoshea kidole cha lawama kundi la Allied Democratic Forces (ADF) kwa shambulizi hilo.

Msemaji wa polisi, Fred Enanga, amesema vikosi vyao vya pamoja vilichukua hatua mara tu baada ya kupokea taarifa na wanawasaka washukiwa waasi wa kundi la ADF.