1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Polisi ya Uganda yatibua njama ya waasi kulipua makanisa

16 Oktoba 2023

Polisi ya Uganda imetibua njama ya shambulizi la bomu lililopangwa na waasi wa ADF dhidi ya makanisa.

https://p.dw.com/p/4XZBA
Polisi wa Uganda walipata duru kuhusu njama ya shambulizi dhidi ya makanisa na wakatibua njama hiyo
Polisi wa Uganda walipata duru kuhusu njama ya shambulizi dhidi ya makanisa na wakatibua njama hiyoPicha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Hayo yamesemwa jana Jumapili na rais wa Uganda Yoweri Museveni kupitia ukurasa wake wa X, awali ukijulikana kama Twitter.

Museveni ameeleza kuwa waasi wa ADF, walitengeneza mabomu mawili waliyokuwa wakipanga kuyatega kwenye makanisa yaliyoko Kibibi na Butambala, umbali wa kilomita 50 kutoka mji mkuu wa Uganda, Kampala. Lakini mabomu hayo yaliripotiwa kwa polisi ambao waliyaharibu.

Mapema Jumapili, Museveni alisema vikosi vyake vilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za ADF katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Museveni ametahadharisha kuwa waasi wa ADF ambao pia wana mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, wanaweza kufanya vitendo vya kigaidi nchini Uganda, kufuatia mashambulizi ya anga dhidi yao.