1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tunisia yawakamata washukiwa ajali ya boti ya wahamiaji

2 Oktoba 2024

Mamlaka za Tunisia zimewakamata watu 12 ikiwa ni pamoja na wanaoshukiwa kuhusika na kuwavusha wahamiaji kwa kutumia boti iliyozama na kusababisha vifo vya watu 15.

https://p.dw.com/p/4lL9P
Tunisia |  Sfax
Wahamiaji wakiwa kwenye mji wa Sfax, Tunisia, kungojea boti za kukimbilia Ulaya.Picha: Yassine GaidiAnadolu/picture alliance

Kwa muijbu wa kikosi cha walinzi wa pwani nchini humo, kiongozi wa walanguzi hao na mkewe walikuwa miongoni mwa waliokamatwa.

Mamlaka pia zimeyakamata magari matatu, boti na kiasi kikubwa cha fedha.

Soma zaidi: Watunisia 12 wafa maji wakikimbilia Ulaya

Rais Kais Saied wa Tunisia, anayewania awamu ya tatu katika uchaguzi unaofanyika siku ya Jumapili, ameiagiza wizara ya mambo ya ndani kulichunguza tukio hilo aliloliita la kuumiza na la ajabu.

Boti hiyo ilizama siku ya Jumatatu ikiwa na wahamiaji 60 karibu na kisiwa cha Djerba na walinzi wa pwani wamewaokoa watu 31 na bado wanawatafuta watu wengine.