1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watunisia 12 wafa maji wakikimbilia Ulaya

30 Septemba 2024

Takribani raia 12 wa Tunisia wakiwemo watoto watatu wamepatikana wakiwa wamekufa baada ya mashua iliyokuwa inawasafirisha wahamiaji kuzama katika pwani ya kisiwa cha kusini mashariki cha Djerba hii leo alfajiri.

https://p.dw.com/p/4lFgZ
Wahamiaji kwenye mpaka wa Libya na Tunisia.
Wahamiaji kwenye mpaka wa Libya na Tunisia.Picha: Yousef Murad/AP/picture alliance

Msemaji wa shirika la misaada la Medenine,  Fethi Baccouche, aliliambia shirika la habari la AFP  kwamba miongoni mwa waliokufa ni wanaume watano na wanawake wanne na chanzo cha kuzama chombo hicho cha baharini bado hakijajulikana.

Soma zaidi: Wahamiaji 28 waliotelekezwa waokolewa Tunisia

Watu wengine 29 waliokolewa kwenye ajali hiyo baada ya walinzi wa pwani ya Tunisia kuarifiwa na wahamiaji wanne waliofanikiwa kuogelea hadi ufukweni.

Tunisia na nchi jirani ya Libya zinatumiwa sana na wahamiaji wanaokwenda kutafuta maisha bora barani Ulaya, mara nyingi wakihatarisha maisha yao katika Bahari ya Mediterania.