Tshisekedi akamilisha ziara yake nchini Burundi
23 Mei 2022Akiwa nchini Burundi rais Tshisekedi alipata fursa ya kutembelea miradi ya ushirika inayofanywa na mataifa hayo mawili, ikiwemo kilimo na ufugaji.
Mbali na miradi hiyo pia kumekuwana miradi ya ambayo inachangia pakubwa maendeleo ya kikanda, ikiwemo ujenzi wa reli kutoka Tanzania, Burundi hadi nchini kwake DRC.
Kwa muda wa siku 3 za ziara yake nchini humu rais Felix Tschisekedi alikuwa na mazungumzo ya ana kwa anma na mwenzike wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Mazungumzo yaliolenga kuhakikisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili unazidi kuimarika.
Soma zaidi:DRC: Yazindua kampeni ya chanjo ya Ebola
Rais Evariste Ndayishimiye amemuhakikishia utayarifu wa serikali yake katika kuiwezesha DRC kupata ujuzu Burundi ilio nao katika sekta mbali mbali.
Suala lausalama lapewa kipaumbele
Marais hao wawili waliangazia juu ya usalama maeneo ya mpakani na hususan kwenye ziwa Tanganyika, na kwenye barabara pamoja na kuahakikisha mikakati ya kurahisisha ubadilishani bidha kati ya nchi hizi mbili.
Rais Felix Tschisekedi alisema mazungumzo yao yamedhamiria maslahi ya nchi hizi 2 na raia wake na manufaa ya muda mrefu kwa raia wake kijamii na hata kibiashara.
"Lazima nchi zetu ziwe na ukaribu na kubuni miradi ya pamoja ya maendeleo." Alisema rais Felix.
Alisisitiza kuwa wamefanya majadiliano mapana katioka suala zima la kuangalia suala la usalama katika matafa hayo jambo ambalo ni kipaumbele kikubwa kwao kwa kuangalia haswa namna majeshi ya nchi hizo yatakavyofanyakazi.
"Tutaangalia jinsi jeshi lilivyo andaliwa hapa ili tuweze kuyaweka mbioni nchini kwetu"
Burundi yaahidi ushirikiano zaidi na DRC
Rasi Evariste Nayishimiye alimuhakikishia mwenzake wa DRC kwambataifa lake lipo tayari kushirikiana kikamilifu katika nyanja ya maendeleo na linapokuja suala la usalama.
"Serikali ya Burundi imejianda kuwafanyia raia wa nchi zetu mbili ili usalama wa watu na vitu uimarike"
Mbali ya mji mkuu Bujumbura rais Felix Tschesekdi alitembelea jumapili hii mji mkuu wa kisiasa Gitega aliko zuri miradi ya kilimo ufukaji, na mshirika ya mshikamano yalojumuika kayika shirikisho la VASO.
Soma zaidi:Asasi za kiraia DRC zalaani ongezeko la mauaji
Nao wake wa marais hao wawili walizuru mkoani hapo Gitega kituo kinacho wapa matibabu wanawake walojifunguwa na kupatwa maradhdi ya kutoweza kuzuwiya haja ndogo, na kuwapatia msada wa vyangula na vitenge.
Ziara hii ya raia Felix T wa DRC imefanyika wakati ni miezi 3, rais wa Burundi Evariuste Nddayishimiye alipo ifanya ziaramjini Kinshasa, na kufuatiwa na DDRC kukubaliwa kuwa mwanachama wa Jumuia ya Afrika mashariki.