1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asasi za kiraia DRC zalaani ongezeko la mauaji

Mitima Delachance19 Aprili 2022

Asasi za kiraia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinalaani kuongezeka la mauaji yanayofanywa na wanajeshi wa serikali, ambao zimewashutumu kuwa na tabia ya kufyatua risasi kwa raia wasio na hatia.

https://p.dw.com/p/4A6Ds
Symbolbild Weltbevölkerungsbericht Frauen
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Hayo yanafuatia kisa cha hivi karibuni katika mkoa wa kivu kusini ambapo askari mmoja wa jeshi la Kongo, FARDC ameuwa watu 7 na kujeruhi wengine 9 kwa kuwafyatulia risasi kule Kazimia, ndani ya wilaya ya Fizi jumatatu.Mapigano yazuka kati ya waasi na jeshi la Congo

Vyanzo mbalimbali kutoka Fizi vinaeleza kuwa mkasa huu ulitokea kufuatia ugomvi uliozuka kati ya polisi na askari waliokuwa kwenye boti moja iliokuwa ikisafirisha wafanyabiashara, abiria wa kawaida, polisi na askari waliorudi kutoka soko la Kazimiya Jumatatu, na kwamba muda mfupi baada ya mabishano askari huyo aliyekuwa afisa wa jeshi la maji aliyeitwa Lukusa Kabamba, alimfyatulia risasi polisi na watu wengine waliokuwepo.

Tosha July ambaye ni mkazi wa Kazimia, amesema wananchi wanapitia masaibu mengi ikiwemo ukandamizwaji  unaofanywa na wanajeshi ambao wanapaswa kuwalindia usalama.

Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
Wanajeshi wa jeshi la Congo FARDCPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Jumapili, mwanajeshi mwingine aliyekuwa mlevi aliua watu wanane (8) wakiwemo wanajeshi wenzake watatu na raia watano kule Bambu katika mkoa wa Ituri mashariki ya Congo.

Asasi za kiraia zinaelezea wasiwasi kuhusu kujirudia kwa visa vya mauaji yanayofanywa na wanajeshi walevi au wenye msongo wa mawazo, zikitaka haki itendeke.Waasi wa ADF wafanya mauaji huko Ituri DRC

Jeshi la Congo FARDC limesema limesikitishwa na tukio la hivi Karibuni kule Kazimia. Msemaji wake kusini mwa mkoa wa Kivu Kusini, Luteni Marc Elongo, amesema kitendo hicho ni cha "kibinafsi" cha askari huyo aliyekosa nidhamu, na ambacho hakiwezi kulihusu jeshi zima.

Pamoja na kutoa rambirambi kwa familia za waathirika, luteni Elongo amesema uongozi wa jeshi la Congo eneo hilo utahakikisha kisa kama hicho hakitokea tena siku zijazo.