1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Yazindua kampeni ya chanjo ya Ebola

Hawa Bihoga
27 Aprili 2022

Shirika la Afya ulimwenguni WHO limesema jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza kutoa chanjo ya Ebola ili kukomesha mripuko wa ugonjwa huo katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Mandaka.

https://p.dw.com/p/4AW0Z
Elfenbeinküste | Impfaktion gegen Ebola
Picha: Sia Kambou/AFP/Getty Images

Hadi sasa WHO imethibithisha watu wawili  kufariki katika mji huo  ulio na wakaazi zaidi ya milioni moja. Kifo cha kwanza kilitokea April 21, huku kifo cha pili kikitokea siku ya jumanne katika mripuko huo wa 14 kutokea  katika taifa hilo lililopo Afrika ya kati, kifo hiki kimehusishwa moja kwa moja na kifo cha kwanza kwakuwa marehemu wote walikuwa ni ndugu.

Mgonjwa wa kwanza alianza kuonesha dalili mnamo April 5, lakini hakutafuta matibabu kwa zaidi ya juma moja. baada ya hapo alilazwa katika kituo cha matibabu ya Ebola mjini Mbandaka mnamo April 2, alifariki siku hiyo baadae.

Soma Zaidi: Mgonjwa wa pili wa Ebola DRC amefariki dunia

 WHO imethibitisha kwamba takriban dozi 200 za chanjo aina ya rVSV-ZEBOVzimesafirishwa hadi katika mji wa Mbandaka kutoka katika mji wa Mashariki wa Goma, huku dozi zaidi zikitarajiwa.

Shirika hilo limeongeza kwamba hadi kufikia sasa visa 233 vimethibitishwa na wanaendelea kufuatilia. Timu tatu za chanjo zipo katika maeneo hayo na zitahkikisha watu wote walio kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo wanafikiwa na mapango huo wa chanjo.

Mkurugenzi wa WHO Afrika Matshidiso Moeti katika tamko lake amesema kwamba pamoja na kuwa na chanjo zinazofaa na uzoefu wa wahudumu wa afya nchini Jamhuri ya Democrasia ya Congo katika kushughulikia Ebola, wanaweza kubadilisha kwa haraka muelekeo wa mripuko huo na kufanikiwa kuudhibiti.

Virusi hivi vimeshindwa kudhibitiwa DCR?

Misitu ya Ikweta ya Kongo ni hifadhi ya asili ya Virusi vya Ebola, ambavyo viligunduliwa karibu na Mto Ebola huko

Kongo Beni Ebola-Opfer
Timu ya wafanyakazi wa afya ikibeba mwili wa aliefariki kwa EbolaPicha: Jerome Delay/AP/picture alliance

Kaskazini mwa Kongo mwaka 1976. Nchi hiyo imeshuhudia awamu 13 za milipuko ya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni pamoja na ule wa mwaka 2018-2022 katika maeneo ya mashariki na kuuwa watu takriban 2,300, ikiwa ni kiwango cha pili cha juu kurekodiwa katika historia ya magonjwa ya homa ya damu.

Soma zaidi:Mripuko mpya wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Congo

Mlipuko wa  karibuni zaidi uliisha mnamo mwezi Decemba  mwaka uliopita katika eneo la mashariki na kusababisha vifo vya watu sita. Mbandaka, mji mkuu wa jimbo la  Ikweta, pia ilishuhudia milipuko mnamo 2018 na 2020.

Uchunguzi mpya wa vinasaba unaonesha kwamba mlipuko wa sasa ni aina mpya ukitajwa kitaalamu Spillover event ikiwa na maana kwamba unasambazwa kutokana na wanyama walioathirika ukilinganishwa na wimbi lililopita ambao haukuhusisha wanya ambao waliathirika.

DR Kongo yaripoti maambukizi mapya ya Ebola