1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiJapan

Tokyo yakumbwa na tetemeko la ardhi la ukubwa wa 5.3

21 Machi 2024

Majengo yametikiswa katika mji mkuu wa Japan, Tokyo baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.3 katika kipimo cha Ritcha na kina cha kilomita 50. Mamlaka hata hivyo haijatoa onyo la kutokea kwa Tsunami.

https://p.dw.com/p/4dxNS
Tahadhari ya kutokea Tsunami yatolewa Japan
Tahadhari ya kutokea Tsunami yatolewa JapanPicha: Tosei Kisanuki/The Yomiuri Shimbu/AP/picture alliance

Idara ya hali ya hewa ya Japan imesema tetemeko hilo limepiga eneo la kusini mwa Ibaraki, mashariki mwa mji mkuu Tokyo.

Televisheni ya shirika la utangazaji la Japan, NKH, imesema hakuna uharibifu au majeruhi walioripotiwa japo mamlaka imesimamisha usafiri wa treni kati ya Tokyo na Koriyamam, katika eneo la kaskazini mashariki mwa Fukushima kutokana na hitilafu ya umeme.

Soma pia: Waliokufa kwa tetemeko Japan wafikia 62 

Japan hukumbwa na takriban mitetemeko ya ardhi 1,500 kila mwaka, idadi hiyo ikiwa asilimia 18 ya matetemeko yote ya ardhi duniani.

Hata hivyo, mingi ya mitetemeko hiyo haina madhara.

Mapema mwaka huu, nchi hiyo ilikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.6 kwa kipimo cha Richter na miji iliyoathirika zaidi ni Toyama, Ishikawa na Niigata, yote kwenye kisiwa chake kikubwa cha Honshu katika mwambao wa magharibi wa Bahari ya Japan.