SiasaAsia
Waliokufa kwa tetemeko Japan wafikia 62
3 Januari 2024Matangazo
Tetemeko kubwa la ardhi lililofikia kipimo cha 7.6 katika jimbo la Ishikawa lilisababisha mawimbi ya tsunami yenye urefu wa zaidi ya mita moja, na kusababisha moto mkubwa na kusambaratisha barabara.Katika eneo la Noto, uharibifu ulijumuisha majengo yaliyoharibiwa na moto, nyumba kusambaratishwa, boti za uvuvi kuzama au kusombwa ufukweni, na barabara kuu zilizovunjika na maporomoko ya ardhi. Shirika la habari laJapanKyodo limeripoti watu walokufa wamefikia 57. Mwaka 2011, nchi hiyo kwa upande wa kaskazini/mashariki ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la ukubwa wa 9.0 katika kipimo cha Richter, ambalo lilisababisha tsunami iliyosababisha vifo vya takriban watu 18,500.