Japan: Idadi ya vifo yapindukia 40 baada ya tetemeko
2 Januari 2024Matangazo
Zaidi ya watu 40 wamekufa baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Japan lililofikia kipimo cha 7.6katika jimbo la Ishikawa.
Televisheni ya Japan, NHK imeripoti kuwa miongoni mwa waliokufa walikuwa watu saba waliokuwapo kwenye hospitali ya manispaa katika mji wa Wajima ambapo majengo zaidi ya 200 yaliteketea kwa moto.
Maafisa wa serikali wanahofia kuwa watu kadhaa wamefunikwa chini ya mabaki ya majengo. Waziri mkuu wa Japan, Fumio Kishida amesema madhara yaliyosababishwa na tetemeko hilo ni makubwa na amesema idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka.
Waziri Mkuu Kishida amesema jambo la kipaumbele ni kuokoa maisha ambapo wanajeshi wapatao 1000 wamepelekwa kwa ajili ya shughuli za uokozi.