1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoNigeria

Nigeria nje, Uingereza yapeta Kombe la Dunia la Wanawake

7 Agosti 2023

Baada ya dakika 120 za mchezo wa hatua ya 16 bora, Nigeria imetupwa nje ya mashindano ya Kombe la Dunia na Uingereza kwa penati 4-2.

https://p.dw.com/p/4UqtS
WWCup Nigeria vs England
Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria wakihuzunika baada ya kutupwa nje na Uingereza katika mchezo wa hatua ya 16 biora.Picha: Tertius Pickard/AP/picture alliance

Timu ya taifa ya Nigeria ya wanawake imeyaaga rasmi mashindano ya Kombe la Dunia la Wanawake yanayoendelea huko nchini Australia na New Zealand baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti na Uingereza 4-2.

Dakika 90 za mchezo wa hatua ya 16 bora ya England na Nigeria hazikutosha kumpata mshindi na kupelekea kuongezwa dakika zingine 30 ambazo pia hazikufua dafu na kupelekea kuumaliza michezo kwa mikwaju ya penati ambayo imepeleka kilio kwa Nigeria.

WWCup Nigeria vs England Chloe Kelly na Alex Greenwood wakishanglia baada ya kupeta hatua ya robo fainali dhidi ya Nigeria.
Wachezaji wa Uingereza Picha: Tertius Pickard/AP/picture alliance

England ambao ndio mabingwa wa Ulaya walicheza na wachezaji 10 pekee katika muda wa nyongeza baada ya mshambualiaji wao Lauren James, mfungaji bora aliyefunga mabao matatu katika hatua ya makundi, kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 87 kwa kumchezea vibaya Michelle Alonzi.

Nigeria ilikuwa ni timu ya kwanza kutoka Afrika kuweka rekodi ya kufika hatua ya 16 bora kabla ya Afrika ya Kusini na Morocco kufuatia. 

Kwa matokeo hayo sasa England iliyo katika nafasi ya nne kwa viwango vya ubora duniani vya FIFA itamenyana na Jamaica au Colombia katika robo fainali huko Sydney siku ya Jumamosi.