1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Theluji yakatisha safari za ndege Munich

2 Desemba 2023

Kutokana na kuanguka kwa kiwango kikubwa cha theluji safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Munich nchini Ujerumani zimesimamishwa hadi kesho saa 12 Asubuhi.Abiria watakiwa kutosafiri kabisa.

https://p.dw.com/p/4Zi39
Flash-Galerie Schneechaos Deutschland November 2010
Kiwanja cha ndege cha Munich kilivyofunikwa na theluji.Picha: AP

Msemaji wa wa uwanja huo pia amesema hata kabla ya kuanza kwa safari hizo tena kesho lakini abiria watapaswa kuangalia ratiba kama upo uwezekano wa safari husika kwa ndege ambazo wanatarajia kusafiri nazo. Uwanja wa ndege wa Munich, ni wa pili kwa shughuli nyingi nchini Ujerumani, na zaidi ya safari za ndege 150 zimesitishwa safari kutokana na kadhia hiyo.Kwa mujibu wa Taasisi ya Huduma ya Hali ya Hewa ya Ujerumani, baridi kali itaendelea kwa wakati huu. Na utabiri unaonesha kiwango kikubwa cha theluji kinatarajiwa kuendelea katika maeneo ya kusini na kusini-mashariki.