1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Utapiamlo watishia kizazi kijacho cha Afghanistan

Angela Mdungu
4 Aprili 2024

Tatizo la utapiamlo nchini Afghanistan kwa kiasi kikubwa limechangiwa na msukosuko uliosababishwa na kundi la Taliban kuingia madarakani mnamo mwaka 2021.

https://p.dw.com/p/4eOfH
Afghanistan | utapiamlo
Mtoto wa miezi 18 anayeugua utapiamlo AfghanistanPicha: Michal Przedlacki/ Save the Children

Kwa mujibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali, kupungua kwa misaada ya kimataifa na uhaba wa madaktari nchini humo kumedhoofisha mfumo wa afya ambao tayari uko hatarini huku wanawake na watoto wakiathirika zaidi. UN: Ukatili dhidi ya watoto waongezeka pakubwa 2020

Lishe duni imekuwa tatizo kubwa katika taifa la Afghanistan linalokabiliwa na migogoro ya kiuchumi, kibinadamu na hali ya hewa ikiwa sasa ni miaka miwili na nusu tangu kundi la Taliban liliporejea madarakani. Umoja wa Mataifa unaripoti kuwa, asilimia kumi ya watoto chini ya miaka mitano nchini humo wana utapiamlo na asilimia 45 wamedumaa.

Afghanistan watoto wenye utapiamlo
Watoto wenye utapiamlo wakiwa kituo cha afya AfghanistanPicha: Bilal Guler/AA/picture alliance

Mkuu wa idara ya mawasiliano wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF,  Daniel Timme anasema, Aghanistan ni moja ya nchi zenye kiwango kikubwa zaidi cha watoto wenye udumavu walio chini ya miaka mitano. Amesema kuwa ikiwa hali hiyo haitogundulika au kupatiwa matibabu ndani ya miaka miwili ya maisha ya mtoto, basi hali hiyo haiwezi tena kutibiwa. Kisha, mtoto aliyeathiriwa kamwe hawezi  kukua kiakili na kimwili kama inavyotakiwa.

Timme  anaongeza kuwa hali hiyo si tu ni janga kwa mtoto husika bali pia ina athari mbaya kwa maendeleo ya taifa zima ikiwa zaidi ya watoto wawili kati ya watano wameathiriwa.  UNICEF; Watoto milioni 7 wanakabiliwa na utapiamlo

Mwanamama Hasina, mwenye miaka  22, pamoja na mume wake Nureddin ni wafanyakazi wa kujitolea katika moja ya mamia ya vituo vya afya vya kijamii vinavyoungwa mkono na shirika la kimataifa la kuwahudumia watoto kwenye eneo la Badakhshan. Eneo ni hilo lenye milima na linapakana na Pakistan, Pakistan, Tajikistan na China. Wanandoa hao wanategemewa kutoa huduma za afya na zaidi ya  wakaazi 1,000 wa kijiji cha Gandanchusma.

Afghanistan
Mtoto akipewa matone ya virutubisho huko KabulPicha: picture-alliance/AP/R. Maqbool

Wanatumia chumba kilichojengwa kwa matope kwenye nyumba yao wanayoitumia kama kliniki. Mara kadhaa, wanawake hufurika wakiwa wamewabeba watoto wao ambao wana utapia mlo.UN: Watoto wengi wameuwawa Afghanistan 2016 Hasina anasema wanawakusanya wanawake hao  na kuwapima watoto wao uzito. Kama wakigundua wana utapia mlo, wanawasaidia kwa kuandikia barua kwenda kwenye kliniki nyingine ambayo kwa mujibu wa Hasina iko umbali wa kilomita 30 kutoka kwenye kliniki yao.Afghanistan kuanza kampeni ya kutoa chanjo ya polio

Muuguzi wa hospitali ya Baharak aitwaye Samira anasema kuwa wakati wa majira ya joto wodi za wagonjwa zinafurika kiasi kwamba wakati mwingine, wanalazimika kuwalaza wagonjwa wawili kwenye kitanda kimoja. Hata hivyo anasema mafunzo wanaopewa juu ya namna ya kuwasaidia wanawake kuwanyonyesha watoto namna ya kuwanyonyesha watoto wao yamesaidia kushusha kiwango cha utapia mlo.UN: Watoto zaidi 8,000 waathirika na vita

Afghanistan Kabul
Mama akiwa na mtoto wake wa mwaka mmoja hospitalini KabulPicha: JORGE SILVA/REUTERS

Chini ya utawala wa Taliban. wanawake wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa vikwazo ambavyo Umoja wa Mataifa umeviita kuwa ni ubaguzi wa kijinsia na wamewatenga mbali na maisha ya umma ya kila siku. Katika ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, iliyotoa tahadhari kuhusu udhaifu wa sekta ya afya ya Afghanistan ilisisitiza madhara hasa kwa wanawake kwa sababu ya vikwazo walivyowekewa katika mienendo yao, elimu na ajira.UN: Mizozo huwauwa na kuwaumiza watoto 12,000

Baadhi ya wanawake wanaoishi kwenye eneo hilo wanasema ni vigumu kupeana taarifa za kiafya hasa katika ngazi ya kijji kwani kuna wanawake wengi ambao hawakusoma. Wanasema, wanahitaji wahudumu wengi zaidi wa afya na wa kijamii ili wazidi kuwahamasisha watu, kugawa dawa kwa watoto wenye utapia mlo na kutoa ushauri kwa wakaazi kuhusu uzazi wa mpango na huduma ya afya kwa ujumla.