1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF; Watoto milioni 7 wanakabiliwa na utapiamlo

23 Mei 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) limesema watoto milioni saba chini ya umri wa miaka mitano nchini Kenya, Somalia na Ethiopia wanakumbwa na utapiamlo.

https://p.dw.com/p/4RhQT
Jemen Unterernährung
Picha: Mohammed Hamoud/AA/picture alliance

Zaidi ya watoto milioni 1.9 katika nchi hizo wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha.

Soma pia: Zaidi ya nusu ya watoto wanakabiliwa na utapiamlo Malawi

Eneo hilo limekumbwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 40. Pia, kutokana na mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo, watu walio katika mazingira magumu wamelazimika kuyahama makazi yao ili kutafuta chakula na maji safi.

Soma pia: Marekani kusaidi watoto wenye utapiamlo, Kenya

Taarifa ya Unicef imeendelea kusema kuwa watoto katika Pembe ya Afrika wanaishi maisha duni kutokana na mgogoro wa njaa, kupanda kwa bei za vyakula, uhaba wa maji safi na usalama mdogo. Aidha Unicef imesema watu milioni 23 wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula katika nchi hizo tatu za Kiafrika huku idadi ya watoto wenye utapiamlo wanaohitaji msaada ikiongezeka.