1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban yakataa kushirikiana na UN ikisema ni upinzani

30 Agosti 2024

Wizara ya Maadili ya Serikali ya Taliban imesema haitashirikiana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, akiutaja kama "upande wa upinzani".

https://p.dw.com/p/4k7JJ
Afghanistan Taliban | Diplomasia |  Waziri wa Mambo ya Ndani Sirajuddin Haqqani.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Taliban Sirajuddin Haqqani.Picha: Siddiqullah Alizai/AP/picture alliance

Taliban inatoa tangazo hili baada ya ujumbe huo, UNAMA, kuonya kwamba sheria mpya ya maadili inayowataka wanawake kujifunika mwili mzima na kutopaza sauti, huenda ikavuruga matarajio ya ushirikiano na jumuiya ya kimataifa.

Soma pia:Ujerumani yawatimua wahalifu wa Afghanistan

Wizara hiyo imeyataka mashirika ya kimataifa, mataifa na watu binafsi wanaoipinga sheria hiyo kuheshimu misingi ya dini ya Kiislamu na kujizuia na ukosoaji na matamko yanayokashifu maadili na utakatifu wa Kiislamu.