1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaChina

WHO yaiomba China kuiarifu zaidi juu ya chanzo cha corona

17 Septemba 2023

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya ulimwenguni, WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameitolea wito China kutoa taarifa zaidi juu ya chanzo cha maradhi ya UVIKO-19.

https://p.dw.com/p/4WRap
Wafanyakazi wa afya wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona mjini Beijing, China, Disemba 9, 2022.
Wafanyakazi wa afya wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona mjini Beijing, China, Disemba 9, 2022.Picha: Ng Han Guan/AP/picture alliance

Ghebreyesus ameliambia gazeti la Financial Times hii leo kwamba wanaendelea kuishinikiza China kuwapa fursa kamili ya kuchunguza na wanayaomba mataifa wanapokutana kwenye mikutano na Beijing, kuiomba kutoa ushirikiano.

 Aidha Ghebreyesus amesema yuko tayari kupeleka timu nyingine kuchunguza suala hilo.

Anatoa matamshi hayo wakati mamlaka za afya na makampuni ya dawa kote ulimwenguni yakiwa yanapambana kuboresha chanjo za kudhibiti aina mpya ya virusi vya UVIKO-19.

Virusi vya corona kwa mara ya kwanza viligunduliwa katika mji wa Wuhan nchini China Disemba, 2019 na kusambaa kote ulimwenguni na kusababisha vifo vya watu karibu milioni 7.