WHO kujadili kitisho cha UVIKO-19
4 Mei 2023Matangazo
Mkutano huo unajiri zaidi ya miaka mitatu tangu kamati hiyoilipotangaza tahadhari ya juu zaidi ya shirika la Afya duniani kuhusu mripuko wa virusi vya UVIKO vilivyoanzia China.
Haijajulikana wazi wataalam wa kamati hiyo wataegemea upande upi. Lakini katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na baadhi ya ishara kwamba shirika la Afya Duniani liko wazi kutangaza mwisho wa dharura ya afya kutokana na UVIKO.
Wiki iliyopita, shirika la WHO lilisema vifo kutokana na UVIKO-19 vimepungua kwa asilimia 95 tangu mwanzo wa mwaka, lakini lilitahadharisha kwamba virusi hivyo bado vinasambaa.