1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO : Maelfu washeherekea kifo cha Pinochet

11 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkI

Maelfu ya wananchi wa Chile wamekuwa wakisheherekea kifo cha dikteta wa zamani wa nchi hiyo Augusto Pinochet ambaye amefariki hapo jana akiwa na umri wa miaka 91.

Mapigano yamezuka huku kukiwa na furaha hiyo ambapo baadhi ya waandamanaji walipambana na polisi karibu la Kasri la Rais.Katika picha nyengine tafauti juu ya kumbukumbu ya utawala wa kikatili wa Pinochet kuanzia mwaka 1973 hadi mwaka 1990 wafuasi kadhaa wa dikteta huyo walikuwa wanaomboleza nje ya hospitali ambako alifariki.

Pinochet anashutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu za madarzeni ya watu lakini hakuwahi kusimama kizimbani kujibu mashtaka kutoka na afya yake kuwa mbaya.Takriban watu 3,000 kwa mujibu wa takwimu rasmi waliuwawa au kuteswa wakati wa utawala wa Pinochet.

Hata hivyo wafuasi wa Pinochet wanampongeza kwa sera zake za kupiga vita ukomunisti.Msemaji wa serikali ya Chile anasema dikteta huyo wa zamani atazikwa kwa heshima za kijeshi na kwamba hakutakuwa na mazishi ya kitaifa.