Ruto asema maandamano ya Kenya lazima yakome
21 Julai 2024Matangazo
Rais William Ruto akionya kwamba machafuko yanaweza "kuharibu" nchi.
Raila amependekeza kwamba kila mwathirika wa ukatili wa polisi alipwe fidia na haki itendeke kabla ya mazungumzo.
Soma pia: Rais wa Kenya amerejea sehemu kubwa ya mawaziri wa zamani
Licha ya Ruto kuondoa sera ya nyongeza ya kodi, maandamano yameendela kwa wiki kadhaa kote nchini Kenya na sasa upinzani umeitisha maandamano mapya wiki ijayo.
Leo Jumapili Ruto ameahidi kuwakomesha "waporaji" na "wauaji" ambao amesema ni "hatari na unaharibu nchi " akiongeza kwamba wanataka taifa lenye amani na utulivu, na masuala ya Kenya yatatatuliwa kwa njia za kidemokrasia.