1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier kuzuru kamati ya Shirika la Msalaba Mwekundu

7 Februari 2023

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anatarajiwa kuitembelea kamati ya kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu mjini Geneva leo.

https://p.dw.com/p/4NBOi
Deutschland Bundespräsident Steinmeier
Picha: John Macdougall/Pool via REUTERS

Rais wa Ujerumani atakabidhi tuzo ya kazi bora kwa aliyekuwa mwenyekiti wa shirika hilo Peter Maurer. Tuzo hiyo inatolewa kwa watu wanaofanya kazi bora za kijamii. Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu inatoa misaada kwa watu walio kwenye maeneo ya migogoro na vita.

Shirika hilo linaendesha kampeni ya kushinikiza utekelezaji wa sheria ya kimataifa juu ya ubinadamu kwa mfano kuhusu madai ya uhalifu wa kivita unaotendwa na majeshi ya Urusi nchini Ukraine. Kamati hiyo imeshiriki katika zoezi la kubadilishana mateka wa vita kati ya Urusi na Ukraine.

Katika ziara yake, rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier pia atafanya mazungumzo na wawakilishi wa asasi ya kamati ya msalaba mwekundu inayoshughulikia vita kati ya Urusi na Ukraine. Pia atakutana na kamishna wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya haki za binadamu Volker Türk.