1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Biden ashinikizwa kuchukua hatua dhidi ya Iran

31 Januari 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anazidi kukabiliwa na shinikizo la kisiasa kuchukua hatua ya moja kwa moja dhidi ya Iran baada ya kuuliwa wanajeshi watatau wa Marekani na wengine wengi kujeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4bmnm
Washington | Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Jonathan Ernst/Pool/File Photo/REUTERS

Tukio hilo la mashambulizi lilifanywa na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran katika eneo la Kaskazini mwa Jordan karibu na mpaka wa Syria siku ya Jumapili.

Rais Joe Biden amesema atachukuwa hatua za kulipiza kisasi ingawa hakufafanuwa zaidi juu ya hatua zitakazochukuliwa.

Wanasiasa wa chama cha Republican wanamshutumu Rais Biden wakisema anasababisha wanajeshi wa Marekani kuwa dhaifu akisubiri mpaka watakaposhambuliwa kwa droni au kombora.

Vikosi vya Marekani katika Mashariki ya kati vimeshambuliwa zaidi ya mara 150 na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran katika nchi za Iraq, Syria, Jordan na kwenye pwani ya Yemen tangu vilipozuka vita kati ya Israel na Hamas mwezi Oktoba.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW