Polisi ya DRC yatawanya maandamano dhidi ya vikosi vya EAC
18 Januari 2023Polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetumia nguvu kutawanya maandamano yaliyofanyika katika mji wa Gom mashariki mwa nchi hiyo, kupinga uwepo wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika eneo hilo.
Watu wapatao 100 walikuwa wamekusanyika karibu na makutano ya barabara tayari kuandamana dhidi ya vikosi hivyo wanavyovishutumu kushindwa kufanya kazi. Miezi ya hivi karibuni, maelefu ya wanajeshi wa Kenya na Burundi walipelekwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulisaidia jeshi la nchi hiyo pamoja na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kupambana na makundi ya waasi katika eneo hilo lenye machafuko.
Mmoja wa waandamanaji Josue Waalay kutoka vuguvugu la vijana wanaharakati, amesema wanajeshi wa Afrika Mashariki hawafanyi chochote zaidi ya kuwalinda aliowaita maadui.