Polisi wa Kenya walizuiwa kuripoti vifo wakati wa maandamano
20 Julai 2023Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la habari la The Associated Press kwamba waliagizwa kutoripoti juu ya vifo chochote cha waandamanaji watakaoshiriki maandamano ya wiki hii ambayo yatahitimishwa kesho Ijumaa.
Afisa huyo ambaye hakutaka kutambulishwa kwa kuwa hakuwa na ruhusa ya kuzungumzia suala hilo hadharani.
Shirika huru la madaktari wa kujitegemea la Kiama limesema angalau watu sita wameuawa jana kwa kupigwa risasi na polisi na wengine 27 waliuliwa katika mazingira kama hayo tangu kuanza kwa mwaka huu. Katika maandamano ya wiki iliyopita, maafisa wa polisi walithibitisha kuwaua watu sita.
Kwa muda mrefu sasa, mashirika ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakishutumu polisi ya Kenya kwa kutumia nguvu kupita kiasi huku kukiwa na wasiwasi juu ya mbinu zinazotumiwa na maafisa hao chini ya utawala wa Rais William Ruto, aliyechaguliwa mwaka jana.
Soma Zaidi: Zaidi ya waandamanaji 300 washikiliwa na polisi nchini Kenya