Zaidi ya waandamanaji 300 washikiliwa na polisi nchini Kenya
20 Julai 2023Matangazo
Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji ndiyo chanzo cha vifo hivyo kufuatia maandamano yaliyoitishwa na viongozi wa upinzani ambao wamedai kuwa maandamano hayo yataendelea.
Shule za kutwa zimefunguliwa tena baada ya serikali kuhakiki hali ya usalama wa wanafunzi. Kwa upande wao, vinara wa upinzani wa Azimio la Umoja bado hawajaonekana hadharani ila wanasisitiza maandamano yanaendelea.
Wito wa kukaa kwenye meza ya mazungumzo bado unatolewa kuwarai kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga na Rais William Ruto kufikia mwafaka.
Serikali imesema vitendo kadhaa vya uharibifu wa mali na wizi vimeripotiwa.