1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Papa Francis ahimiza mazungumzo kumaliza mzozo wa Sudan

23 Aprili 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ametoa wito hii leo wa mazungumzo kati ya pande zinazohasimiana katika mapigano nchini Sudan yanayoingia wiki ya pili sasa.

https://p.dw.com/p/4QSUk
Italien Rom | Papst Franziskus verlässt Krankenhaus
Picha: Remo Casilli/REUTERS

Papa Francis amenukuliwa hii leo akirudia tena wito huo kutokana na hali ya usalama kuzidi kuzorota na kutaka mapigano kusitishwa mara moja. Amesema hayo wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro huko Roma.

Aidha amemuomba kila mmoja kuendelea kuwaombea watu wa Sudan.

Soma Zaidi:Sudan: Guterres atoa wito wa kusitishwa mapigano 

Mataifa ya kigeni kama Marekani, Ufaransa, Italia na Uturuki yamewaondoa raia wao nchini humo kutokana na mapigano hayo yanayohusisha jeshi rasmi la Sudan dhidi ya lile la Dharura, RSF. Watu zaidi ya 400 wameripotiwa kuuawa hadi sasa na wengine kukimbilia nchi jirani kama Chad.