1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Nigeria yakabiliwa na kitisho cha maandamano wiki hii

29 Julai 2024

Nigeria inakabiliwa na kitisho cha maandamano makubwa ya nchi nzima wiki hii ya kupinga hali ngumu ya kiuchumi.

https://p.dw.com/p/4is7n
Waandishi wa habari wakikimbia usalama wao baada ya polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji nchini Kenya.
Waandishi wa habari wakikimbia usalama wao baada ya polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji nchini Kenya. Picha: Boniface Muthoni/SOPA/IMAGO

Wanasiasa na jeshi la nchi hiyo wametowa tahadhari kwa wananchi dhidi ya kuingia mitaani ingawa waandaaji wa maandamano hayo wamesema kushindwa kwa serikali ndiko kumewafanya kukosa namna nyingine.

Japo bado haijafahamika maandamano hayo yatachukuwa sura gani lakini yamefananishwa na kile kilichotokea hivi karibuni nchini Kenya.

Maandamano makubwa nchini Kenya ya vijana yaliilazimisha serikali ya Rais William Ruto kuondowa muswaada wa nyogeza ya kodi. Maandamano ya nchini Nigeria yamepangwa kuanza Alhamisi wiki hii.

Soma pia: Jeshi la Nigeria laonya dhidi ya ghasia za mtindo wa Kenya

Wakati huo huo, polisi nchini Uganda wanaendelea na operesheni ya kuwakamata vijana wanaondamana kupinga ufisadi nchini humo huku Rais Yoweri Museveni akiahidi kuwapa msahaha vijana waliokamatwa ikiwa watawafichua watu wanaowafadhili.

Takriban watu 104 kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters wamekamatwa kufuatia maandamano.

Wengi waliokamatwa wamefunguliwa mashtaka ya kuvuruga usalama wa  umma kwa mujibu wa taarifa ya polisi. Vijana nchini Uganda walioanzisha maandamano hayo, hata hivyo wamemkosoa Rais Museveni. 
 

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW