1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yafanya juhudi za kuwaokoa wanafunzi waliotekwa

Sylvia Mwehozi
9 Machi 2024

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametuma vikosi vya majeshi kuwaokoa zaidi ya wanafunzi 250 waliotekwa nyara na watu waliojihami kwa bunduki kutoka shule moja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4dKaX
Nigeria
Gari ya maafisa wa usalama katika eneo walikotekwa wanafunzi NigeriaPicha: AP/dpa/picture alliance

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametuma vikosi vya majeshi kuwaokoa zaidi ya wanafunzi 250waliotekwa nyara na watu waliojihami kwa bunduki kutoka shule moja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Rais Tinubu ameelezea matumaini kwamba wanafunzi hao wataokolewa na haki itapatikana.

Tukio hilo lililotokea kwenye jimbo la Kaduna ni la pili katika utekaji nyara watu wengi ndani ya kipindi cha wiki moja katika taifa hilo hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika. Magenge ya wahalifu waliojihami kwa pikipiki huwalenga raia katika vijiji na shule na kando ya barabara kuu katika msako wa malipo ya fidia.Zaidi ya wanafunzi 280 watekwa nyara Nigeria

Wiki iliyopita kulitokea utekaji nyara mwingine kwenye jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, katika kambi ya watu walioachwa bila makao kutokana na machafuko yanayosababishwa na wanamgambo wenye itikadi kali.